Standard (EADGBE)

Intro

, , , x3

Verse 1

Kidum)

Ikiwa umeamua kunitoroka

Ikiwa unahisi kwamba hujiskii nami tena

Na mbona imekuwa ngumu kunidokeza

Naona ni bora nilie leo, badala ya kesho

Kupendwa, usipendwe ni kama kujitia kitanzi

Nitachimba na sururu kwa ardhi, nikitafuta penzi lako

Pre-chorus

Kidum)

Ni heri nipigwe fimbo kwa mwili

Sababu nitajikuna, ama nitajikanda na maji moto

Maumivu ya penzi, mtu hajikuni

Wala hajikandi na maji

Na hakuna upasuaji (yoii yoo)

Chorus

Kama kuna kosa, nimewahi fanya (nieleze)

Kama kuna jinsi, tunaweza leta (mpaka niishi)

Na kama kuna kitendo, linaweza tendwa (nieleze)

Nitafanya, fanya, Nitatenda, tenda

Nitafanya, fanya, Nitatenda, tenda

Nitafanya (nasema), fanya, Nitatenda, tenda

Nitafanya, fanya, Nitatenda, tenda (woohh)

Verse 2

Lady Jaydee)

Kweli hukumbuki ulioyafanya

Ni kweli unakumbuka tulikotoka

Sisemi habari zozote za kusikia

Bali kwa ushahidi, niliouona

Msamaha mara ngapi? umeshaomba na bado

Je, ni makosa mangapi? niliyoyafumbia macho

Pre-chorus

Lady Jaydee)

Mpaka leo nahisi kufika kikomo

Maumivu yanazidi ndani ya moyo

Sitaki kwenda mbali kwani upo moyoni

Nikusamehe mimi mara ngapi wewe?

Nieleze mpenzi mara ngapi?

Chorus

Unataka, nikusamehe mara ngapi? (usihesabu)

Unapenda nikuvumilie mara ngapi? (hii ni ya mwisho)

Je, wewe nikulilie mara ngapi? (vumilia)

Sitoweza (utaweza wee), Nimechoka (usichoke)

Nimeshindwa (usishindwe), Naondoka (usiondoke mamii)

Sitoweza (sitoweza), Nimechoka (usichoke)

Nimeshindwa (usindindwe), Naondoka leo

Bridge

Kidum)

Ukihesabu ni mara ngapi umenisamehe

Ni kama kuhesabu ni mara ngapi mtoto kaharibu nepi

Usichoke, usiondoke, usilie, niko hapa kukulinda

Chorus

Kama kuna kosa, nimewahi fanya (nieleze)

Kama kuna jinsi, tunaweza leta (mpaka niishi)

Na kama kuna kitendo, linaweza tendwa (nieleze)

Nitafanya, fanya, Nitatenda, tenda

Nitado do do do, fanya, Nitafanya, tenda

Nitafanya , fanya, Nitatenda, tenda

Nitado i swear, fanya, Nitafanya, tenda (woohh)

Unataka, nikusamehe mara ngapi? (usihesabu)

Unapenda nikuvumilie mara ngapi? (mara ya mwisho)

Je, wewe nikulilie mara ngapi? (usilie)

Sitoweza (unaweza), Nimechoka (usichoke)

Nimeshindwa (usishindwe), Naondoka (uhh uhh)

Sitoweza (weza), Nimechoka

Nimeshindwa, Naondoka leo

Outro

, , , )

Usishindwe baby

Nitado do do do do