Ad loading…

Standard (EADGBE)

Intro

Ohhh Ohhh, yeahh ehhh

yeahh

Verse 1

Penzi ni kitu ambacho kinaweza kukupa furaha maishani mwako

Vilevile penzi linaweza kukupa huzuni milele moyoni mwako

Ukashindwa kuelewani na ndugu, rafiki hata na wazazi wako

Utakosa raha ya maisha, hata kama una pesa

Vitalala viungo vyako, kimawazo utakesha

Utakosa raha ya maisha, hata kama una pesa

Vitalala viungo vyako, kimawazo utakesha

Chorus

Sumu ya penzi ukishailamba

Hata kwa maziwa huwezi kupona

Sumu ya penzi ukishailamba

Hata kwa maziwa huwezi kupona

Sio kwamba mi nakukataa

Ila moyo wangu unasita (moyo unasita)

Wazazi wangu watanishangaa

Nyumbani wewe ulishatoroka (ulishatoroka)

Sio kwamba mi nakukataa

Ila moyo wangu unasita

Wazazi wangu watanishangaa

Nyumbani wewe ulishatoroka

Verse 2

Ulinimwaga kama mchele, kuku wanidonoe (mimi)

Ukanifunga mpaka kitanzi, nani aniokoe (porini)

Ulinimwaga kama mchele, kuku wanidonoe (mimi)

Ukanifunga mpaka kitanzi, nani aniokoe (porini)

Laiti ningejua kuna dawa ya mapenzi

Ningejifunga nisipende

Maana mapenzi kwangu yamekuwa shubiri

Kwa wenzagu mitende

Laiti ningejua kuna dawa ya mapenzi

Ningejifunga nisipende

Maana mapenzi kwangu yamekuwa shubiri

Kwa wenzagu mitende (yeahh)

Chorus

Bridge

Mi sihitaji mapenzi na wee

Mi sitaki mapenzi na wee

Ohh baby naomba unielewe

Mi sitaki mapenzi (sihitaji) na wee

Nachoweza kusema, sihitaji mapenzi na wee

Nachoweza kusema, sihitaji mapenzi na wee

Nachoweza kusema, sihitaji mapenzi na wee

Mapenzi na wee (ihhh ihhh)

Sio kwamba mi nakukataa (mi nakukataa)

Ila moyo wangu unasita (moyo unasita)

Wazazi wangu watanishanga (watanishanga)

Nyumbani wewe ulishatoroka (ulishatoroka)

Sio kwamba mi nakukataa (ohh ohh)

Ila moyo wangu unasita (ohh ohh)

Wazazi wangu watanishangaa (ohh ohh)

Nyumbani wewe ulishatoroka (ohh ohh)

Outro

Sio kwamba mi nakukataa aahh (mimi)

Wazazi wangu watanishanga aahh (mimi)

Sio kwamba mi nakukataa ahhh (ihhh ihh)

Wazazi wangu watanishanga ahhh (yeahh)

Belle 9, rocka Tz records

Niko na Triss